KAMBI YA MAZOEZI YA ARGENTINA YAJAWA NA FURAHA IKIWA NA MESSI

Lionel Messi na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Argentina wameonekana kuwa wenye furaha mno katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia 2018 dhidi ya Chile utakaofanyika Santiago.

Nyota huyo anayechezea timu ya Barcelona ya Hispania hakucheza na timu ya taifa tangu Julai 2015, huku akiikosa michezo yote ya kampeni ya kuwania kufuzu michuano, na kuifanya timu hiyo kuwa na wakati mgumu bila yeye.
          Wachezaji wa Argentina wakiwa na furaha wakati wakifanya mazoezi yao
Mazoezi yao yaliambatana na adhabu za mizaha za kuchapana makofi kichwani kama inavyoonekana hapa
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment