March 22 2016 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai
alifanya mabadiliko ya baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge,
huku akiwaondoa wenyeviti na makamu wenyeviti watano katika kamati
walizokuwa wakiziongoza baada ya kuwepo kwa tuhuma nzito za rushwa
zilizohusisha kamati hizo.
Leo March 23 2016 Chama cha ACT Wazalendo
kimetoa msimamo wake juu ya maamuzi yaliyofanywa na Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwahamisha kamati Wenyeviti, Makamu
wenyeviti na Wajumbe wa baadhi ya kamati za kudumu za Bunge uliofanywa
jana March 22 2016
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti, Kamati ya Bunge na Serikali za mitaa, ACT Wazalendo, Yeremia Kulwa Maganja amesema …..
>>>’tangu
mabunge yaliyopita, kamati za Bunge zimekuwa zikituhumiwa mara kadhaa
kujihusisha na vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa mashirika ya Umma,
Makampuni na watu binafsi, uamuzi wa kuwahamisha kamati viongozi ni sawa
na kuufunika uozo, hili linaendeleza utamaduni mbovu wa siku nyingi
hapa nchini wa kuwahamisha au ‘kuwapangia kazi nyingine’ viongozi na
watumishi wa umma wanaotuhumiwa kupokea rushwa au kukosa ufanisi‘
>>>’Chama
cha ACT Wazalendo kinamtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuitisha mara moja uchunguzi kwa kamati zote zilizotuhumiwa ili
ukweli ubainike na hatua zichukuliwe mara moja’
0 comments:
Post a Comment