Stori za joto kuongezeka kipindi hiki sehemu mbalimbali duniani zimekuwa zikichukua headlines kubwa sana, ilianza Dubai joto lilipanda mpaka nyuzi 38, tukasikia Uingereza nako nyuzi joto liligonga 40 ikaja India pia joto nyuzi lilifikia nyuzi 45.
Nimekutana na sotri kutoka Italy ambako nyuzi joto limeongezeka kufikia nyuzi 37C…matukio
na athari za jua yamekuwa yakiweka headlines mbalimbali Italy moja wapo
ni hii ya gari kuyeyuka kutokana na joto kali la jua.
Tukio
lilinaswa kwenye picha na video na mtalii mmoja aliyekuwa anatoka
hotelini kuelekea beach na kisha kushangazwa kuona uji uji mzito
unidondoka kutoka kwenye gari hilo, alipolikaribia gari hilo aligundua
kuwa gari lilikuwa linayeyuka kutokana na joto kali la jua.
Kitu hiki
kimewashangaza watu wengi huku vyombo vingi vya usalama nchini humo
vimewaomba watu kupunguza kutoka nje na kwenda baharini na kufunga
viyoyozi vitakavyowasaidia kupunguza joto.
Hapa chini nimekuwekea kipande cha video kinacho onyesha gari hilo likiyeyuka.
0 comments:
Post a Comment