Faisal Azim wa Chittagong,Bangladesh alikuwa wa pili na picha yake kuhusu watu watatu waliojaa vumbi katika timbo ya mchanga.
Nafasi ya tatu ni picha ya ngamia iliopigwa na Ahmed Al Toqi wa Musact Oman.Alipata fursa muhimu wakati wa mashindano ya ngamia hao.
Picha nyengine saba pia zilituzwa ikiwemo picha ya Sarah Wouters ya vijana wawili waliokuwa wakijaribu kulishika bata ndani ya maji katika mkoa wa Nong Khai nchini Thailand.
Matokeo hayo yaliafikiwa baada ya raundi mbili za ukaguzi wa ubunifu na picha zilizotoka kwa ubora zaidi.Ndani ya chumba cha kuoga na mvuke kilichopo mita 2800 juu ni picha iliopigwa na Stefano Zardini.
''Usiku wa kuamkia picha hii,tulijaribu kupata picha nzuri ya faru weupe walio katika hatari ya kuangamia'', alisema mpiga picha Stefane Berube.''Nikijaribu kujificha katika nyasi ili kuwa umbali wa futi 30 sikufanikiwa kupata picha niliotarajia.hatahivyo nilipata picha ya faru watatu waliokuwa malishoni''.
Picha ya Alain Schroeder inaonyesha kushti- jina jingine la mchezo wa mieleka nchini humo.Baada ya mazoezi washiriki hupumzika wakitegemea kuta za jukwaa kwa kuficha miili na vichwa vyao kwa mchanga ili kuzuia kupigwa na baridi.sherehe hiyo ya kupumzika hufuatiliziwa na masaji ya kunyoosha misuli iliochoka pamoja na kuonyesha heshima.
Mwengine aliyehitaji kutuzwa ni Eduard Gutescu kwa picha yake ya barafu juu ya kijiji cha Pestera ilioitwa Ardhi ya Romania iliojaa hadithi chungu nzima.
''Usiku kabla ya kurudi mjini Windhoek,tulitumia saa kadhaa katika eneo la Deadveli'',alisema mpiga picha Beth McCarley.Mwezi uliokuwa uking'ara vizuri kumwilika mchanga uliojaa kwa umbali,lakini mbingu zilikuwa na giza na haikuwa rahisi kuona njia na mawingu ya Magellanic.
Picha ya Batlomiej Jurecki ya utamaduni wa kutengeza nyasi nchini Poland ambapo watu wengi wanaendelea kutumia jembe lenye meno ili kutawanya nyasi hizo.
0 comments:
Post a Comment