James Mbatia
ni mmoja wa Viongozi wa Umoja wa UKAWA, August 20 2015 amekutana na
Waandishi wa Habari kwenye Ofisi za Makao Makuu ya NCCR- Mageuzi, Ilala
Dar.
Kazungumzia kuhusu ishu ya UKAWA kuzuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwenye uzinduzi wa Kampeni zao, Uchaguzi na kutoonekana kwa Dk. Slaa.
>>> “Kampeni
zinaanza nawasihi Wanasiasa wote wachunge ndimi zao sana, tujadili hoja
kwa hoja kwenye majukwaa ya kisiasa sio kujadili watu, matusi, wala
kupigana ngumi au kumwaga damu… Tume ya Uchaguzi ambayo ndio refa itende
haki pamoja na vyombo vya dola… Wakitenda haki hakuna mgogoro wa aina
yoyote, Kamati za Ulinzi na Usalama Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya
hatutaki waingilie mchakato huu.“
Kuhusu kuzuiwa Uwanja wa Taifa Dar majibu yake ni haya>>> “Uwanja
wa Taifa ni mali ya Watanzania, tutakutana tutatafakari alafu
tukishakubaliana kwa pamoja tutatoa taarifa wapi tutakutana na
tutazungumza nini, kwa kweli hatuna majibu mpaka sasa hivi“– James Mbatia.
Haya ndio Majibu ya James Mbatia kuhusu ishu ya Dk. Slaa kutoonekana kwenye Vikao vya UKAWA >>> “UKAWA
sio Mbatia, sio Slaa sio Lipumba sio Mbowe… tusijadili watu tujadili
hoja za msingi za taifa, watu wanapita, tuzungumzie Watanzania zaidi“
P yhaa tv coming soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

0 comments:
Post a Comment