POLISI NCHINI KENYA IMETOA PICHA YA MKE WA MPIGANAJI WA AL-SHABAAB

Polisi nchini Kenya imetoa picha ya mke wa mpiganaji wa Al-Shabaab anayetafutwa kwa mashambulizi ya mabomu ya kutupa kwa mikono na mauaji mjini Mombasa.

Polisi pia imetenga zawadi ya shilingi milioni 2 za Kenya, kwa mtu atakayetoa taarifa itakayosaidia kukamatwa kwa mwanamke huyo Rukia Mbarak Faraj, ambaye ni mke wa Ramadhan Kufungwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi Faraj anahusika na tukio la mashambulizi ya kutumia mabomu ya kutupa kwa mkono na anahisiwa kuwa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi kaskazini mashariki mwa Kenya.
P yhaa tv coming soon

Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
 


face book ipyana stephen






  Share


















usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos 





Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment