Pictured: Oscar Pistorius 'playing football in PRISON yard with alleged ...



Haya mengine yaliendelea jela Pistorious alikofungwa… Hasira, chakula? Sumu.. Choo na bafu?


Jail Pisto
Toka Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela ni October 2014,
huenda yapo mengi yaliyoendelea ndani ya gereza na hukupata nafasi
kuyajua… Kwa Sheria za South Africa ziko stori toka ndani ya Gereza watu
wan je wanaweza kuzipata tofauti na Sheria za nchi nyingine !!


Cha kwanza ni kwamba kumbe jamaa alikuwa
mtu mwenye hasira sana siku za kwanza kwanza alivyoanza kutumikia
kifungo chake, Maafisa Magereza wawili waliopata nafasi kuwa karibu nae
zaidi wamesema wakati huo hakutaka hata kuongea na mtu yoyote wakati
huo.


Siku za kwanza alikuwa anatumia mpaka
saa 23 za siku nzima kukaa ndani ya chumba chake jela bila kuongea na
mtu yoyote, wala kutoka nje, baadae akaanza kuzoea… >>> ‘Sasahivi ni mtu anayeweza kuongea na kucheka na mtu yoyote’—hii ni nukuu ya alichokisema Ngobeni, mmoja wa Maafisa Magereza hao.


Kingine ni kwamba kuna wakati alidai
anataka kujengewa bafu lake mwenyewe kwenye chumba chake, akajengewa
bafu pamoja na choo cha pekeyake.. akadai abadilishiwe kitanda,
akabadilishiwa. Akataka abadilishiwe vifaa vya gym yake, navyo
vikabadilishwa.


Kuna stori ambayo hii ni moja ya
zilizosambaa sana mitandaoni kwamba alikuwa na hofu ya kuwekewa sumu
kwenye chakula, akabadilishiwa chakula… alihitaji chakula chake kiwe
kinanunuliwa kwenye Duka la Magereza.


Siku chache zilizopita baada ya kuwepo kwa stori kwamba huenda akaachiwa huru na kutumikia kifungo che nje, Pistorious aliyasema haya >>> ‘Nimeikumbuka Familia yangu… natamani kuwa nao karibu zaidi, nina hamu ya kuwaona’.


Pistorious anatumikia kifungo ndani ya Gereza la Kgosi Mampuru II, Maofisa ambao wamekuwa nae karibu zaidi na kutoa stori hizo ni Violet Ngobeni na Boitumelo Morake.


Hiki ni kipande cha video kilichowahi kutoka kikionesha Pistorious akicheza mpira Gerezani.
P yhaa tv come soon















Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE


share
 
















face book ipyana stephen











































































Share





































































































































































































































































usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos 













































































































































Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment