Ikulu ya White House, makazi rasmi ya rais wa Marekani
Kumeapishwa marais 43, na kumekuwa na marais 44, kwa sababu rais Grover Cleveland alihudumu mihula miwili isiyofuatana, na kwa hivi anahesabiwa mara mbili, kama rais nambari 22 na nambari 24. Marais wanne walifariki kawaida wakiwa mamlakani (William Henry Harrison, Zachary Taylor, Warren G. Harding, na Franklin D. Roosevelt), mmoja akajiuzulu (Richard Nixon), na wane wakauawa (Abraham Lincoln, James A. Garfield, William McKinley, na John F. Kennedy). Rais wa kwanza wa Marekani alikuwa George Washington, aliyeapishwa 1789 bada ya kupigiwa kura na wajumbe wote katika kongamano. William Henry Harrison alihudumu kwa muda wa siku 31 pekee, mwaka 1841, naye Franklin D. Roosevelt akahudumu kwa muda mrefu zaidi kuliko wote, miaka 12. Rais wa sasa in Barack Obama, aliyeapishwa 20 Januari 2009.
0 comments:
Post a Comment