Bilionea mjasiriamali, Elon Musk huenda akafanya hadithi za kusadikika kutoka kwenye vitabu vya sayansi kuwa kweli, kwa kuwezesha binadamu kusafiri kwa haraka zaidi ndani ya bomba lililopunguzwa hewa kabisa (vacuum) zinazoweza kwenda kwa spidi kubwa zaidi ya ile ya ndege. Bomba ilo pamoja na vyombo vyake vya usafiri kufahamika kama Hyperloop.
Usafiri wa aina tofauti kabisa
Ujenzi
wa majaribio wa bomba hilo huenda ukaanza kufanyika mapema mwakani, na
majaribio ya mwanzo kutazamiwa kufanyika katika bonde la Quay, huko
Califonia mwaka 2018 na kugharimu Dola Milioni 100 kwa kuanzia.
Bilionea, Bwana Elon Musk.. Mdhamini na mwekezaji mkuu wa teknolojia hii
Kampuni
ya Hyperloop Transportation Technologies wanataka kuthibitishioa dunia
kuwa hilo linawezekana, kwa kuingia ubia na mashirika mengine kama
kampuni ya ubunifu wa ukandarasi ya AECOM na Shirika la Uswisi la
Oerlikon ambalo limejikita katika teknolojia za utupu
(Vacuum-technology) ambao ndio mhimili wa mradi huu.
Mchoro unaoonesha jinsi wasafiri watakavyoweza kukaa katika chombo hicho cha usafiri
Mtandao maarufu wa teknolojia wa Wired, ulioripoti kuhusu mwanzo wa mradi huu kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Itajuhuhisha ujengwaji wa miundombinu spesheli kabisa
Dhana
ya mwanzo ya mradi huo inaonyesha ganda la nje, mfano wa gari dogo
lenye siti za abiria likiwa ndani ya bomba(tube) ya aluminiam. Nguvu ya
umeme itatumika kuendesha usafiri huu. Kwa usafiri huu, umbali wa
Kilomita hadi 600 (Karibu na Umbali wa Arusha hadi Dar es Salaam) huenda
ukafikiwa kwa muda wa NUSU saa tu! Ndio, Nusu saa tu.
Mkufunzi
mmoja wa mambo ya usafiri amesema huenda mradi huu ukabakia kuwa dhana
kutokana na vikwazo kama milima pamoja na gharama.
Musk
mwenyewe amesema amejikita zaidi katika mradi wa majaribio, na
amesisitiza kuwa utakuwa wa wazi kwa yeyote atakayekuwa tayari kutaka
kuuendeleza.
Vyanzo; Al-Jazeera, TheStar.com, ETE na Google Image
P yhaa tv coming soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

0 comments:
Post a Comment