Mchawi wa Barcelona, Lionel Messi ameonekana mtulivu kwenye mazoezi ya jana akijiandaa na mechi ya UEFA Super Cup.
Siku
chache zilizopita, Messi alicheza dhidi ya AS Roma katika mechi ya
kirafiki dhidi ya AS Roma ya Italia, lakini ndani ya uwanja kulikuwa na
cheche za aina yake.
Messi alimpiga kichwa na kumkaba koo beki wa Roma, Mapou Yanga-M'Biwa, Barcelona ikishinda 3-0 Camp Nou.
Muargentina huyo hakuoneshwa kadi nyekundu kwa kufanya tukio hilo.
Andres Iniesta na Gerard Pique wakitembea wakati wa mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Boris Paichadze Dinamo Arena
Straika wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez akionesha vitu vyake wakati wa mazoezi
Kocha
wa Barcelona, Luis Enrique anatarajia kuanza kukusanya makombe usiku wa
leo ambapo anashuka dimbani kuchuana na Sevilla katika mechi ya UEFA
Super Cup, huku akimtegemea mchawi wake Messi.
0 comments:
Post a Comment