Baada ya kuzidiwa kete na kocha wa
Chelsea Jose Mourinho na kumkosa mshambuliaji wa Barcelona Pedro,
kocha wa Manchester United Louis van Gaal sasa ameelekeza nguvu zake
kumnasa Sadio Mane wa Southampton.
Tayari timu ya Southampton imekiri
kupokea maombi ya Manchester United ya kutaka kumtwa Mane aliyefunga
mabao 10 katika michezo 32 ya Ligi ya Kuu ya Uingereza msimu uliopita
baada ya kununuliwa kwa kitita cha paundi milioni 10 kutoka Red Bull
Salzburg.
Kama hiyo haitoshi van Gaal pia
amepigwa kumbo na majirani wake Manchester City baada ya kufanikisha
kumtwaa beki wa Valencia Nicolas Otamendi kwa ada ya uhamisho wa
paundi milioni 32.

P yhaa tv come soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos



0 comments:
Post a Comment