Yvonne Chaka Chaka andika haya kuhusu collabo ya Alikiba na mwanamuziki mkongwe wa nchini Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka.
Wimbo huo ambao tayari unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa muziki Afrika hususan wa Alikiba, ulirekodiwa jijini Johannesburg. Alikiba tayari ameshaelezea hisia zake baada ya kufanya kazi na muimbaji huyo na kueleza kuwa ni heshima kubwa kwake.
“It was a great honor and pleasure to meet Mama Yvonne Chaka Chaka who I have loved and admired all my life,” aliandika kwenye Instagram.
“Thank you for hosting us and sharing your memories, advices and guidance. I am truly grateful and looking forward to our project,” aliongeza.
Na sasa Yvonne naye ametumia Instagram kuelezea collabo hiyo. Amedai kuwa amefurahi kufanya kazi na hitmaker huyo wa Aje.
Yvonne Chaka Chaka aliyezaliwa kwa jina, Yvonne Machaka mwaka 1965, ni mwanamuziki anayeheshimika zaidi Afrika Kusini huku pia akijihusisha na masuala ya misaada ya kibinadamu na ualimu.
Alipewa jina la ‘Princess of Africa’ kwa mafanikio makubwa kimuziki aliyoyapata kwa miaka 27. Nyimbo zake zilizotamba ni pamoja na I’m Burning Up, Thank You Mister DJ, I Cry for Freedom, Makoti, Motherland na Umqombothi ambao ulitumika kwenye filamu ya mwaka 2004, Hotel Rwanda.
0 comments:
Post a Comment