
Uchaguzi huo unafanyika wakati ambapo mpinzani mkuu wa Rais John Mahama, Nana Akufo-Addo akiwa analalamika kuhusu demokrasia iliyokandamizwa nchini humo. Mshindi katika uchaguzi huo ataiongoza Ghana kwa kipindi cha miaka minne ijayo. Kiasi ya watu milioni 15 wamejiandikisha kupiga kura. Vituo vya kupigia kura vinafunguliwa saa moja kamili asubuhi kwa saa za Ghana na vitafungwa majira ya saa 11 jioni. Kuna wagombea saba katika kinyang'anyiro hicho na iwapo vyama vidogo vitafanya vizuri na kusababisha wagombea wakuu kutopata wingi wa kura zinazohitajika, basi duru ya pili ya uchaguzi itafanyika mwishoni mwa mwezi huu. Mahama mwenye umri wa miaka 58, anagombea kwa muhula wa pili, huku Akufo-Addo mwenye umri wa miaka 72 akiwa anashiriki kwa mara ya tatu.
0 comments:
Post a Comment