Man United wakiwa ugenini wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, ushindi wa Man United ulithibitika dakika ya 88 baada ya Zlatan kupachika goli la ushindi, kwani kabla ya hapo matokeo yalikuwa 1-1, hiyo ni baada ya goli la dakika ya 45 lililofungwa na Paul Pogba kusawazishwa na James Mcarthur dakika ya 66.
Ushindi huo unakuwa ushindi wa 7 wa Man United msimu huu katika Ligi Kuu Englandbaada ya kucheza mechi zake 16, huku wakiwa wametoa sare 6 na kuruhusu kufungwa michezo mitatu, Man United sasa atacheza mchezo wake wa 17 wa EPL December 17 2016 dhidi ya West Bromwich Albion.
0 comments:
Post a Comment