UN: Boko Haram yasababisha watoto laki nne kukabiliwa na utapiamlo Nigeria
Umoja wa Mataifa umesema kuwa zaidi ya watoto laki nne wanakabiliwa na utapiamlo nchini Nigeria kwa sababu ya mapigano ya Boko Haram na robo yao huenda wakafariki mwakani.
Shirika la kuwahudumia watoto duniani UNICEF limetaja sehemu zilizo athirika zaidi kuwa ni jimbo la Borno, huku robo tatu ya maji na pamoja na miundombinu ikiwa imeharibiwa ama kutokuwepo kabisa.
Umeonya kuwa magonjwa ya kuharisha pamoja na malaria yanaongezeka yanayohatarisha zaidi maisha ya watoto.
0 comments:
Post a Comment