Timu ya Southampton imefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la EFL kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1987, kufuatia kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Arsenal.
Magoli kutoka kwa Jordy Clasie ambaye ni goli lake la kwanza kwa klabu yake na la Ryan Bertrand yaliipa Southampton ushindi wa kwanza dhidi ya Arsenal katika msimu huu.
Meneja Arsene Wenger, ambaye hajawahi kushinda kombe hilo alifanya kosa la kuwapumzisha wachezaji wake 10 muhimu, kosa ambalo lilimgharimu.
Jordy Clasie akiachia shuti na kufunga goli la kwanza
Ryan Bertrand akifunga goli la pili la Southampton
0 comments:
Post a Comment