
Timu za FC Barcelona na Real Madrid zote ziliingia zikiwa na kumbukumbu kuwa mchezo wao wa mara ya mwisho kumalizika pasipo goli ilikuwa ni mwaka 2002, huku Real Madrid waliingia kutetea rekodi yao ya kucheza mechi yao ya 33 bila kuruhusu kupoteza mchezo hata mmoja na kutoka sare mechi 7 pekee.

December 3 2016 katika uwanja wa Nou Camp mchezo huo wa El Clasico umemalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, FC Barcelona ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 53 kupitia kwa Luis Suarez na Real Madrid wakafanikiwa kusawazisha goli dakika ya 90 kupitia kwa Sergio Ramos.

Msimamo wa LaLiga baada ya matokeo ya mechi ya FC Barcelona vs Real Madrid
0 comments:
Post a Comment