PROF. LIPUMBA: “BODI YA WADHAMINI CUF ACHENI KUTAFUTA HURUMA YA KISIASA, HAMUWEZI SHINDA KESI HII”

lipumba

Baada ya shauri namba 23/2016 lililofunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msajili wa Vyama vya Siasa na Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF anaetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na wenzake.
Na kuahirishwa hadi Disemba 14, 2016 kufuatia mawakili upande wa wadaiwa kukataa maombi ya upande wa wadai ambao ni Bodi ya Wadhamini CUF ya kumuomba Jaji Sakieti Kihiyo anayeisimamia shauri hilo kujiondoa katika usimamizi kwa sababu mbalimbali kutojibiwa..
Prof. Lipumba ambae ni mshitakiwa namba tatu katika shauri hilo, amewata viongozi wa CUF kutolitumia shauri hilo kupata huruma ya kisiasa na kudai kuwa kuna dalili za Bodi ya Wadhamini CUF kushindwa katika kesi hiyo na kwamba wanaitumia hoja ya kumkataa jaji Kihiyo ili shauri lichelewe kusikilizwa na au watakaposhindwa wajitetee kwamba hawakutendewa haki.
“Tufanye shughuli za kujenga chama ili tujipange kwa ajili ya uchaguzi badala ya kupoteza muda mahakamani kwa kesi isiyo na msingi,” alisema na kuongeza.
“Wenyewe walifungua shauri hili kwa hati ya dharula halafu wenyewe wanazuia lisiendeshwe kwa haraka huku wakimtaka jaji ajiondoe pasipo kueleza sababu za msingi za jaji kujitoa.”
Lipumba amedai kuwa, “Jambo la kusikitisha wanatafuta huruma ya kisiasa ili jaji akikataa kujiondoa wakishindwa waseme jaji hakutenda haki ndio maana walimkataa na pia wakifanikiwa kumuondoa wajisifu kuwa wamemuondoa.”
Amesema yeye bado mwenyekiti halali na kuwataka baadhi ya viongozi wanaompinga kuheshimu katiba kwa madai kuwa alichaguliwa kihalali na uenyekiti wake utakoma ifikapo 2019.
“Tumeacha peleka kesi za msingi kama za wawakilishi wetu waliopewa hati za ushindi na kunyimwa uakilishi na kuleta kesi zisizo za msingi za kupoteza muda,” amesema.
Aidha, jana ilikuwa siku ya kusikilizwa na kujibiwa maombi ya wadai yaliyolenga kumkataa jaji anayesimamia kesi hiyo kwa madai kuwa ameonyesha dalili za kuegemea upande mmoja.
Lakini mawakili upande wa wadaiwa wakiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Obadia Kameya, walizipinga hoja kuu mbili zilizotolewa na upande wa wadai kwa madai kuwa hazikuwa za msingi.
Hata hivyo, wakili upande wa wadai Juma Nassoro alijibu hoja za mawakili wa wadaiwa kitendo kilicholeta mvutano na kusababisha Jaji Kihiyo kuahirisha shauri hilo hadi Disemba 14, 2016.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment