DUNIA KUTUMIA DOLA TRILIONI 1.5 KWA DAWA IFIKAPO 2021

murray-aitken



Dunia inatarajiwa kutumia zaidi ya dola za Marekani trilioni 1.5 katika bajeti ya dawa ifikapo mwaka 2021.

Kwa mujibu wa ripoti ya Taasisi ya QuintilesIMS Institute for Healthcare Informatics zinasema kiwango hicho kinaongezeka kutoka kiwango kilichofikiwa mwaka 2016 cha dola za Marekani trilioni 1.2

Hata hivyo imeelezwa kuwa ongezeko hilo linaenda taratibu zaidi sasa kuliko kipindi cha awali ambacho kiliona kuingia katika soko la tiba kwa dawa za kutibu hepatitis C na kansa.

Mkurugenzi Mtendaji wa QuintilesIMS Institute, Murray Aitken, alisema kwamba kiwango cha mseleleko wa bei ya dawa duniani kipindi dawa hizo za kisasa za kutibu kansa zilipoiingia hakikuwa cha kawaida.

Mkurugenzi Mtendaji wa QuintilesIMS Institute, Murray Aitken.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano ijayo hatarajii kasi ya ongezeko la fedha katika tiba kutokana na ukweli kuwa zipo dawa zitajiongeza sokoni katika usajili au kukabiliana na ushindani wa dawa nyingine ambapo kwa namna hiyo hali itakuwa bora zaidi.

Imeelezwa katika tarifa hiyo kwamba hali ya matumizi katika tiba iko sanjari na dawa mpya za tiba zilizothibitishwa nchini Marekani, soko kubwa la dawa duniani, kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2014 na 2015.

Kulikuwa na dawa mpya 45 zilizopitishwa na FDA mwaka jana na mwaka 2014 zilikuwa 41 na mwaka 2016 kufikia Desemba tano dawa mpya zilizopitishwa ni 19.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment