Zlatan Ibrahimovic amefunga goli la dakika mbili kabla ya mchezo kuisha na kuipatia ushindi Manchester United na kuitubulia mambo Crystal Palace.
Raia huyo wa Sweden alifunga akiunganisha mpira wa pasi ya Paul Pogba uliomshinda Wayne Hennessey baada ya goli la James McArthur kuonekana kuipatia pointi Palace.
Pasi ya Pogba ilikuwa kama ni ya kulipa fadhila kwa Ibrahimovic kwa kumtengenezea goli la kwanza lililotumbukizwa na mchezaji huyo raia wa Ufaransa.
Paul Pogba akiifungia Manchester United goli la kwanza katika mchezo huo
James McArthur akifunga goli la kusawazisha hata hivyo Zlatan Ibrahimovic aliongeza la pili
0 comments:
Post a Comment