Tunazihesabu siku tu kabla ya kuachiwa album mpya ya Navy Kenzo ambayo wameipachika jina la Above in a Minute (AIM).
Wiki iliyopita ilitoka list kamili ya ngoma ambazo zitapatikana kwenye album hiyo, na kilicho washangaza wengi ni pale walipoona ngoma kama Kamatia Chini, Chelewa na nyingine kibao ambazo zimewahi kuhit kitaani hazikuorodheshwa kwenye album hiyo.
Perfect255 ikaona sio kesi, wacha tumnyamate Nahreel na kupiga nae story ni vipi kuhusiana na mchongo huo.
“Imewashangaza wengi, lakini sisi tumejaribu kuleta kitu kikubwa na cha tofauti ili watu waone ni kweli tunafanya kazi, tumeiheshimu album. Kwakweli zile ngoma zilitoka kama solo, nadhani isingeleta picha nzuri zingekuwa kwenye album, labda zingekuwa kwenye bonus.” Alisema Nahreel.
Play hii video hapa chini umsikilize Nahreel kiufasaha zaidi akifunguka juu ya mchongo huo.
0 comments:
Post a Comment