

Akizungumza kwenye uzinduzi wa ushirikiano huo wa kimataifa uliofanyika kwenye kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya vijana, Afisa Mkuu wa Biashara wa City Football Group Tom Glick amesema …>>>“Tunafurahi kuwakaribisha TECNO Mobile katika mkusanyiko wa ushirikiano wa kimataifa, kujikita kwake zaidi katika masoko ya nyumbani kunaendana na namna ambavyo tunafanya shughuli zetu na tunatazamia kushirikiana nao kuungana na mashabiki wa Manchester City duniani kote”
Vile vile Mkurugenzi Mtendaji wa TECNO Mobile Stephen Ha alizungumza katika uzinduzi huo wa kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya vijana cha Manchester City kwamba
>>>“Tunashukuru sana kushirikiana na klabu yenye mafanikio na inayojulikana ya Manchester City, tutaendeleza uhusiano wetu wa muda mrefu katika michezo kwa hali ya juu kwa kuwapatia wateja wetu uzoefu wakufurahia zaidi simu bora isiyolinganishwa na nyingine”
0 comments:
Post a Comment