Manchester United itavaana na Hull City katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la EFL, wakati Liverpool ikishuka dimbani kukabiliana na Southampton.
United, ambayo iliifunga West Ham 4-1 jana usiku, watacheza mchezo wao wa kwanza wa nusu fainali katika dimba la Old Trafford.
Southampton, iliyopata ushindi rahisi dhidi ya Arsenal siku ya jumatano, watakuwa wenyeji wa Liverpool katika dimba la St Mary kwenye mchezo wa kwanza wa fainali na kumalizia Anfield.
0 comments:
Post a Comment