Mshambulia wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake mkuu Lionel Messi na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa soka duniani 'Ballon d'Or'.
Ronaldo ameitwaa tuzo hiyo kwa mara ya nne, huku mpinzani wake Messi akiwa ameitwaa tuzo hiyo kwa mara tano ikiwemo mwaka jana.
Messi alishika nafasi ya pili katika tuzo hizo na mshambuliaji wa Atletico Madrid Mfaransa Antoine Griezmann akiwa katika nafasi ya tatu.
Ronaldo aliisaidia Real Madrid kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya, na aliisaidia Ureno kushinda michuano ya Euro 2016.
Ronaldo akiwa na Mama yake Maria na mwanae Cristiano Junior
0 comments:
Post a Comment