Bingwa mara tisa wa Olimpiki Usain Bolt ameshinda tuzo ya IAAF ya Mwanariadha Bora wa Kiume wa Mwaka na kuweka rekodi ya kutwaa tuzo hiyo mara sita.
Mwanariadha wa Ethiopia, Almaz Ayana, aliyevunja rekodi ya mbio za mita 10,000 na kushinda medali ya dhahabu Rio ametwaa tuzo ya Mwanariadha Bora wa Kike.
Bolt, 30, alitwaa medali tatu za dhahabu katika michuano ya Olimpiki ya Rio katika mbio za mita 100, 200 na 4x100.
Mwanariadha Usain Bolt anatarajia kustaafu riadha mwakani
0 comments:
Post a Comment