BESIKTAS YASHUSHIWA MVUA YA MAGOLI NA KUTOLEWA NJE LIGI YA MABINGWA ULAYA


Matumaini ya Besiktas kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana usiku wakati wachezaji wao wawili wakitolea nje huku wakikubali kichapo kikali cha magoli 6-0 kutoka kwa Dynamo Kiev.

Mchezo huo ulianza kuharibika dakika ya 29, pale beki wa Besktas Andreas Beck alipotolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Derlis Gonzalez na Dynamo kupewa penati iliyozaa goli la pili.

Katika mchezo huo Vincent Aboubakar naye alipewa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano na kuzidi kulizamisha jahazi la Besiktas.
                  Junior Moraes akifunga goli la sita la Dynamo Kiev katika mchezo huo
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment