Waendesha mashtaka wanashinikiza kufungwa jela miaka 10 mchezaji wa zamani wa Barcelona Samuel Eto'o kwa tuhuma za kukwepa kodi wakati akichezea klabu hiyo.
Waendesha mashtaka pia wanataka Eto'o kulipa faini ya dola milioni 15.1 kwa makosa manne ya kukwepa kodi, na kuikosesha mamlaka ya kodi ya Hispania dola milioni 4 katika mwaka 2006-2009.
Kama hiyo haitoshi waendesha mashtaka pia wanataka adhabu kama hiyo itolewe kwa muwakilishi wake kwa wakati huo Jose Maria Mesalles Mata.
Samwel Eto'o akiwa na Lionel Messi wakati huo akichezea Barcelona
0 comments:
Post a Comment