ROONEY AWEKA REKODI WAKATI MANCHESTER UNITED IKIIFUNGA FEYENOORD


Wayne Rooney ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa Manchester United kuifungia magoli mengi timu yake katika ligi ya Uropa baada ya kufunga jana katika mchezo na Feyenoord walioibuka na ushindi wa magoli 4-0.

Kapteni huyo wa Red Devils alifunga goli lake la 39 katika michuano ya ligi ya Uropa kwa kuunyanyua mpira juu ya kipa Brad Jones akiunganisha pasi ya uhakika kutoka kwa Zlatan Ibrahimovic.

Rooney pia alimtengenezea Juan Mata goli la pili, na kisha baadaye kipa Jones akajifunga goli la tatu akijaribu kuuokoa mpira uliompita tobo uliopigwa na Ibrahimovic, kabla ya Jesse Lingard kufunga la nne dakika za majeruhi kwa mpira wa shuti la kuzungusha.
                                        Wayne Rooney akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
                                                               Juan Mata akiteleza na kufunga goli la pili
Hii ndio hatari ya kucheza na mchezaji anayecheza Kung fu: Zlatan Ibrahimovic akirusha teke la juu kuupiga mpira ambao hata hivyo aliukosa
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment