UJERUMANI BILA WAKALI WAKE YAIFANYIA MAUAJI SAN MARINO


Winga Serge Gnabry amefunga magoli matatu 'hat-trick' wakati akiichezea Ujerumani kwa mara ya kwanza na kuisaidia kuichakaza San Marino kwa magoli 8-0 jana, katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia.

Ujerumani sasa wameweka rekodi ya kufanya vyema katika hatua ya kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia kwa kushinda michezo minne na kuendelea kuongoza kundi lao, huku wakiwa hawajafungwa goli.

Kocha wa Ujerumani Joachim Low, akishusha kikosi chake bila ya wachezaji wake sita muhimu wakiwemo Jerome Boateng, Manuel Neuer na Toni Kroos, alimpa majukumu winga wa Werder Bremen, Gnabry naye hakumuangusha. 
                     Sam Khedira akiifungia Ujerumani goli la kwanza katika mchezo huo 
  Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Serge Gnabry akiifungia Ujerumani goli la pili katika mchezo huo.

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment