ROONEY ATAKA GARETH SOUTHGATE KUKABIDHIWA RASMI TIMU YA TAIFA


Kapteni wa timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney anataka kocha wa muda Gareth Southgate kupewa moja kwa moja jukumu la kuinoa timu hiyo, kutokana na kuipatia matokeo mazuri.

Rooney ametoa kauli hiyo wakati Southgate akipata ushindi wa pili katika michezo mitatu aliyoiongoza Uingereza, kwa kuifunga jana Scotland katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia.

Katika mchezo huo wa jana Uingereza ilionekana kuwa imara zaidi ya Scotland na kuifunga kwa magoli 3-0, magoli yaliyofungwa na Daniel Sturridge kwa mpira wa kichwa, na kisha Adam Lallana kufunga la pili, Gary Cahill akafunga la tatu kwa kichwa kufuatia mpira wa kona ya Rooney.
           Daniel Sturrige akiwa chini akiangalia mpira wa kichwa alioupiga ukijaa wavuni
   Gary Cahill akiwa ameupiga mpira kwa kichwa ambao ulimshinda kipa wa Scotland na kujaa wavuni
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment