Mchezaji nyota Lionel Messi amefunga moja na kusaidia mengine mawili wakati Argentina ikicharuka katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia dhidi ya Colombia jana usiku.
Nyota huyo wa Barcelona aliifanya Argentina ipate goli la kwanza kwa mpira wa adhabu alioupiga katika dakika ya 10, kabla ya kutengeneza mengine kwa Lucas Pratto na Angel di Maria katika kipindi cha pili.
Ushindi huo wa Argentina umeondoa machungu ya kufungwa magoli 3-0 na Brazil wiki iliyopita, na kufufua matumaini yao ya kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia 2018 itakayofanyika nchini Urusi.
Kipa David Ospina akiruka bila ya mafanikio kuufuata mpira uliopigwa na Lionel Messi
Lucas Pratto akiwa ameachia shuti lililojaa wavuni baada ya kupata pande kutoka kwa Messi
Angel di Maria akiwa ametikisa nyavu baada ya Messi kupasua ngome na kumpatia pasi
0 comments:
Post a Comment