MSANII MATOYA ATAKA KUWAPATANISHA MASTAA ALI KIBA NA DIAMOND


diamondmatonya-na-alikiba
Msanii mkongwe wa muziki nchini, Matonya amedai hakuna kinachoshindikana kama wasanii, viongozi pamoja wadau mbalimbali kwa pamoja wakiamua kuwapatanisha Alikiba na Diamond.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Sugua Benchi’, ameiambia Bongo5 kuwa maelewano kwa wasanii ni kitu ambacho kitaleta tija na msingi mzuri kwa wasanii pamoja na jamii inayowazunguka wasanii.
“Chuki ndo chanzo cha mambo mengi ambayo yanatokea katika hii dunia,” alisema Matonya “Kama unakumbuka katika kipindi cha nyuma kuna wasanii walichomana visu na mmoja akafariki sitaki kulizungumzia kiundani lakini nadhani watu wanaelewa nazungumzia nini,”
“Wasanii wote ni kitu kimoja, tunatakiwa kuungana kwa pamoja ili kuupeleka muziki wetu sehemu fulani, kwa hiyo mimi nadhani kuwapatanisha Diamond na Alikiba haishindikani, tuna viongozi wengi, wasanii kwa pamoja tunaweza kuwaweka sawa na hata wakafanya project ya pamoja,” aliongeza Matonya.
Pia muimbaji huyo alisema atafanya mazungumzo na wadau mbalimbali kuangalia namna ambavyo wanaweza kufanya project ya pamoja ili kurejesha umoja baina ya wasanii hao.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment