Liz Skelcher alikuwa akimnyonyesha manawe wa wiki 11 Evie katika mkahawa wa Nandos wakati kisa hicho kilipotokea wiki iliopita.
Mkahawa huo umesema kuwa unaruhusu akina mama kunyonyesha wana wao
Lakini ilikuwa wateja wengine wa kike waliomtusi mwanamke huyo aliyekitaja kisa hicho kama cha kutisha na kushangaza.
Akizungumza na kpindi cha BBC cha Talkback, bi. Skelcher alisema: Nilikuwa katika mkahawa huo na mumewangu pamoja na mamake mume wangu wakati Evie alipoamka na akataka kunyonya,nilimuinua na kumuweka katika titi moja.Kulikuwa na wanawake watatu katika meza moja na mmoja wao hakupendelea mimi kumnyonyesha mwanangu.
Aliniambia kwamba tulikuwa tunamkera kumyonyesha mtoto katika mkahawa.
Aliendelea kunitusi mbele ya marafikize na alipoulizwa shida yake ilikuwa nini,alisema hakutaka kuona matiti yangu wakati alipokuwa akila chakula chake cha jioni.
0 comments:
Post a Comment