Katika mchezo huo ambao Argentina wameingia uwanjani wakiwa na hali mbaya katika msimamo, kutokana na nafasi waliopo hawezi kucheza Kombe la dunia na watahitaji kushinda michezo kadhaa ili kufufua matumaini ya kucheza Kombe la dunia 2018, wamejikuta wakipigwa goli 3-0 na Brazil.
Kiama cha Argentina kilitolewa na Philip Coutinho dakika ya 29 baada ya kupokea assist safi ya Neymar ambaye baadae alifunga goli la pili dakika ya 45 kwa assist ya Gabriel Jesus, kabla ya Jose Paulinho kukomelea msumari wa mwisho dakika ya 58 uliomfanya Lionel Messi na wenzake watoke vichwa chini uwanjani.
0 comments:
Post a Comment