Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaongoza viongozi mbali mbali wakati wa mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu wa UWT Mhe. Amina Makilagi (kushoto) wakimfariji akimfariji Mama Margaret Sitta (katikati) wakati wa mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
...............................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza viongozi na wananchi katika mapokezi ya Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ukitokea nchini Ujerumani alipofariki wakati anapatiwa matibabu.
Akizungumzia jinsi anavyomfahamu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Taifa limeondokewa kiongozi mwadilifu,mzalendo, mchapakazi na mtetezi wa wanyonge hivyo taifa litaendelea kuumuenzi utendaji wake.
Viongozi mbalimbali waliojumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu Samweli Sitta kweye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere ni pamoja na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Seif Ali Iddi, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika, Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
0 comments:
Post a Comment