MAGOLI 12 YAFUNGWA KATIKA MCHEZO WA BORUSSIA DORTMUND NA LEGIA WARSAW


Borussia Dortmund na Legia Warsaw zimeweka historia katika Ligi ya Mabigwa Ulaya kwa mchezo wao kuwa na matokeo ya kufungwa magoli 12, yakiwa ni idadi kubwa ya magoli kuwahi kutokea katika mchezo mmoja.

Dortmund inayonolewa na Thomas Tuchel iliifunga Legia Warsaw magoli 8-4 katika mchezo ambao utabakiwa kuwa wa kumbukumbu uliochezwa nchini Ujerumani.

Matokeo hayo yanaipiku rekodi ya magoli 11 kufungwa katika mechi moja wakati Monaco ikiifunga Deportivo La Coruna kwa magoli 8-3 mwaka 2003.

Katika mchezo wa jana magoli 7 yalifungwa ndani ya dakika 22 za mwanzo wa mchezo huo. Marco Reus alifunga magoli matatu yaani hat-trick na Shinji Kagawa akifunga magoli mawili.
                                                        Marco Reus akiwa ametumbukiza mpira kimiani
                   Oussmane Dembele licha ya kutegeneza magoli matatu alipachika goli moja
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment