Mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale itabidi asubiri kuona iwapo atakuwa mzima kuweza kucheza mchezo wa El Clasico dhidi ya Barcelona baada ya kuumia jana.
Nyota huyo wa Wale, 27, alitoka akichechemea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya walioshinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Sporting Lisbon akiwa ameumia enka.
Vinara hao wa ligi ya La Liga wanaoongoza kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Barcelona wataenda Nou Camp jumamosi ya Desemba 3.
Varane akiifungia Real Madrid goli la kwanza katika dakika ya 29
Karim Benzema akifunga kwa kichwa goli la ushindi kwa Real Madrid
Gareth Bale akiwa amelala chini akigugumia maumivu ya enka
0 comments:
Post a Comment