Bi. Hillary Clinton amesema kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais Marekani, kumechangiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI).
Bi. Clinton amesema kauli ya Mkurugenzi wa FBI James Comey kuwa wameanzisha uchunguzi mpya dhidi ya tuhuma za kutumia seva ya barua pepe binafsi akiwa Waziri wa Mambo ya Nje ilimpunguzia kasi ya ushindi.
Kauli hiyo ya mgombea huyo wa urais wa chama cha Democratic imenaswa katika maongezi yake kwa njia ya simu na wafadhili wakuu wa chama cha Democratic, na kuvujishwa kwenye vyombo vya habari.
Mkurugenzi wa FBI James Comey
Wakati huo huo maandamano yanaendelea kupinga ushindi wa Dodald Trump katika miji kadhaa ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment