Conor McGregor ameshinda mkanda wa uzito wa lightweight kwa KO katika raundi ya pili dhidi ya Eddie Alvarez katika mchezo wa mapigano ya kutumia ngumi na matake wa UFC 205 Jijini New York, Marekani.
Kwa ushindi huo McGregor ameweka rekodi ya kuwa bingwa wa kwanza wa UFC kutwaa ubingwa wa mikanda miwili kwa wakati mmoja, baada ya hapo awali kuwa na mkanda wa ubingwa wa uzito wa featherweight.
McGregor raia wa Ireland alimuangusha chini mpinzani wake Alvarez mara tatu katika raundi ya kwanza kwa ngumi na mateko mazito yenye uhakika, kabla ya kumaliza shughuli katika raundi ya pili kwa KO.
Conor McGregor akiwa amemtandika ngumi iliyomlevya Eddie Alvarez
Eddie Alvarez akianguka chini baada ya ngumi ya McGregor kumuingia barabara huku refa akimhesabia anyanyuke
Conor McGregorakimpiga ngumi na teke ka ubavuni Eddie Alvarez
Conor McGregor akimpa ngumi ya kwenye kidevu mpinzani wake Eddie Alvarez
0 comments:
Post a Comment