

Mchezo kati ya Arsenal dhidi ya Paris Saint Germain ya Ufaransa ulikuwa ni moja kati ya michezo nane iliyochezwa usiku wa November 23, PSG wakiwa Emirates waliutawala mchezo kwa asilimia 52 dhidi ya wenyeji wao Arsenal waliokuwa wameutawala mchezo kwa asilimia 48.

Arsenal wakiwa nyumbani wamelazimishwa sare goli 2-2, magoli ya Arsenal yakifungwa na Oliver Giroud dakika ya 45 na dakika ya 59 Marco Verratti alijifunga, wakati magoli ya PSG yalifungwa na Edinson Cavani dakika ya 18 na goli lao la pili lilipatikana baada ya beki wa Arsenal Alex Iwobi kujifunga kwa kichwa dakika ya 77.
0 comments:
Post a Comment