Timu ya Barcelona imepoteza nafasi ya kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi Kuu ya Hispania ya La Liga baada ya kuduwazwa kwa magoli 4-3 na Celta Vigo katika dimba la Balaidos.
Iago Aspas alikuwa chachu ya magoli 3-0 katika kipindi cha kwanza, kwa kumtengenezea Pione Sisto goli la kwanza, kufunga la pili na kulazimisha goli la kujifunga la Jeremy Mathieu.
Barcelona walipambana na kurejesha goli kupitia kwa mpira wa kichwa wa Gerard Pique, na penati ya Neymar, huku kosa la kijinga la Marc-Andre ter Stegen kuwafanya Celta kufunga goli la nne. Pique alifunga kwa kichwa goli la tatu la Barcelona.
Mchezaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas akifunga goli la pili la Celta Vigo
Mchezaji nyota wa Brazil na Barcelona Neymar alifunga goli kwa mkwaju wa penati
0 comments:
Post a Comment