Sababu za Wastara kurudiana na mpenzi wake wa zamani


Mwigizaji Wastara aliwahi kuingia kwenye vichwa vya habari Tanzania kutokana na ndoa yake kuvunjika ndani ya siku 80 akiwa kaolewa na Mbunge wa Zanzibar.
Kabla ya ndoa hiyo Wastara alikuwa kwenye uhusiano na mshikaji ambaye ni staa wa Bongo Movie pia ambaye anaitwa Bondi, sasa basi baada ya taarifa kuenea katika mitandao mbalimbali kwamba amerudiana na Bondi leo ameyazungumza haya juu ya taarifa hizo.

Unajua watu hawajui tulipotoka yule ni mtu wangu wa muda mrefu ni makosa yake tu alinikosea ndio sababu ya mimi kuachana naye na ndipo nikaamua kwenda Zanzibar kuolewa yakatokea yaliyotokea na sasa niko na Bondi yaani nimerudiana naye nimesamehe yaliyopita kwasasa tuna kama miezi miwili tangu turudiana katika uhusiano wetu’
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment