Rais Barack Obama amesema msimamo wa mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump wa kusema kuwa huenda asikubali matokeo ya uchaguzi wa rais, ni wa hatari.
Akiongea kwenye mkutano wa kampeni ya mgombea wa urais wa Democratic, Hillary Clinton, huko Miami rais Obama amesema matamshi ya Trump yanaishusha demokrasia ya Marekani.
Trump aligoma kwenye mdahalo wa kwenye TV kusema iwapo atakubali matokeo ya urais ya Novemba 8, iwapo atashindwa.
0 comments:
Post a Comment