Mume wa mwanamuziki wa Marekani, Mary J. Blige, anashinikiza alipwe fedha ya kujikimu dola 130,000 kila mwezi na mkewe ili aendelee kushi maisha ya kifahari, baada ya mkewe kuomba talaka.
Mume huyo Martin 'Kendu' Issacs, 49, anaamini mkewe nyota wa R&B Blige anapaswa kumlipia gharama za mazoezi, mpishi wake binafsi na posho ya dola 1,000 kwa ajili ya kununulia mavazi.
Mary J. Blige, 45, amefungua maombi ya kutalikiana na mumewe Issacs mwezi Julai mwaka huu, kutokana na sababu ambazo amesema haziwezikupatiwa upatanishi, baada ya miaka 13 ya ndoa.
Mary J Blige akiwa na mumewe Martin 'Kendu' Issacs
0 comments:
Post a Comment