Wakati wa mchezo huo mchezaji wa Stand United Abasrim Chidiebere alitolewa nje ya uwanja baada ya kugongwa katika taya na beki wa Azam FC Aggrey Morris, kupitia mtandao wa habari za michezo Tanzania wa shaffihdauda.co.tz umeripoti taarifa ya daktari kuhusu mchezaji huyo.
Nahodha wa Azam FC John Bocco alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji wa Azam FC waliokwenda kumsalimia Chidebere
Kwa mujibu wa shaffihdauda.co.tz Chidebere ambaye kwa sasa hawezi kuongea kutokana na kufungwa nyaya maalum katika meno yake, daktari amesema atakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki mbili kwa ajili ya kuuguza jeraha hilo huku akisisitiza pia anahitaji uangalizi wa karibu kwa wakati huu.
CHANZO: shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment