Msafara wa JPM wakumbana na foleni, mwenyewe ataka kutembea kwa miguu
Katika hali ambayo sio ya kawaida kwa kiongozi kama rais wa nchi, Rais John Magufuli ambaye yupo nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili amekutana na foleni wakati akielekea katika eneo ambalo alizikwa Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, aliuambia mtandao wa Star wa Kenya kuwa Rais Magufuli alikutana na foleni hiyo wakati akitokea katika hoteli ya Intercontinental na kuelekea eneo la alilozikwa Jomo Kenyatta na baada ya kuona kuna foleni kubwa alitaka kutembea ili aweze kufika eneo ambalo anataka kwenda kuliona.
Aidha baada ya kutoka eneo hilo alikuta tayari maafisa wa usalama wameshaweka magari mengine pembeni ya barabara ya Uhuru na hivyo aliweza kupita kwa urahisi kuelekea ikulu kukutana na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta.
Baada ya kuwasili ikulu JPM alionana na Rais Kenyatta na kufanya mazungumzo kisha kulihutubia taifa la Kenya kuhusu mahusiano ya Kenya na Tanzania na mipango ambayo wameiweka baada ya kufanya mazungumzo.
0 comments:
Post a Comment