Nike wameripotiwa kuingia mkataba wa udhamini na Chelsea katika kipindi cha miaka 15, mkataba ambao utawafanya walipwe pound milioni 60 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 155, mkataba huo utawafanya Chelsea wavune jumla ya pound milioni 900 katika kipindi cha miaka 15 ambazo ni zaidi ya Tirioni 2 za kitanzania.
Chelsea watamaliza mkataba wao na Adidas mwezi May 2017, hivyo ni baada ya kukubaliana kuvunja mkataba wao wa udhamini wa miaka 6, mkataba wa Chelsea naAdidas ulikuwa unawafanya walipwe pound milioni 30 kwa mwaka ambazo ni sawa na Tsh bilioni 79.9, kitu ambacho Nike ambao ni wapinzania na Adidas wameongeza mara mbili yake.
0 comments:
Post a Comment