Mario Balotelli mpya amendelea kuonyesha makali yake na kuisaidia Nice kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Nates, na kuifanya timu yake kuongoza Ligi 1 kwa tofauti ya pointi sita.
Mshambuliaji huyo wa Italia, aliyejiunga na Nice akitokea Liverpool, alifunga goli sita katika ligi hiyo na pia kusaidia kupatikana mengine mawili akitakana mno katika dimba la Allianz Riviera.
Kiungo Wylan Cyprien alitikisa nyavu mara mbili na Alassane Plea naye alifunga goli na kuifanya Nice ambayo haijafungwa kuwa na pointi 29 katika michezo 11.
Wylan Cyprien akifunga goli la kwanza la Nice
Super Mario Balotelli akifunga goli huku kipa wa Nates akiwa hana jinsi zaidi ya kuuangalia mpira uliomshinda kuudaka ukitinga wavuni
0 comments:
Post a Comment