KIM KARDASHIAN ALIHOFIA WEZI WALIOMVAMIA HOTELINI PARIS WANGEMBAKA



Kim Kardashian alihofia kuwa huenda angebakwa, wakati taarifa za kuhuzunisha zikiibuka kuwa alifungwa mikono na kuachwa kwenye bafu katika hoteli ya kifahari Jijini Paris na kuibiwa vito vya mamilioni ya dola.

Wakati tukio hilo likitokea jana asubuhi Kim alikuwa amelala na mara akashtuka baada ya kuwasikia wezi hao waliokuwa wamevalia mavazi ya polisi na kufunika sura zao wakipanda ngazi za kwenye jengo alilokodi kwenye hoteli.

Kim, aliwaomba wezi hao wasimuue na kuwaambia kuwa anawatoto wawili wakati wezi hao watano walipomkamata mikono na kumfunga na kumziba mdomo kwa kumfunga na  gundi ya kufungia vifurushi 'duct tape' na kisha kumuacha bafuni.
     Muonekano wa ndani wa jengo la hoteli ambalo Kim alikuwa amelipia kwa malazi Jijini Paris 
               Kim Kardashian akiwa na mumewe Kanye West baada ya kurejea nchini Marekani
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment