Infantino kufanya mabadiliko Kombe la Dunia kwa kuongeza timu shiriki

rais-wa-fifa-infantino



Kama ilivyo kawaida ya kila kiongozi kuwa na namna yake ya uendeshaji wa madaraka ambayo anakuwa amepatiwa, hivyo ndivyo ilivyo kwa Rais wa FIFA, Gianni Infantino ambaye katika awamu yake anataka kufanya mabadiliko kwa kuongeza timu ambazo zinashiriki Kombe la Dunia.

Akiwa katika ziara Bogata, Colombia, Infantino alisema ametoa mapendekezo kwa Baraza la FIFA kutaka kuongeza idadi ya timu ambao zitakuwa zinashiriki Kombe la Dunia lakini zitakuwa zinafanyiwa mchujo na kubakiza timu 32, pendekezo ambalo linataraji kujadiliwa wiki ijayo na kutolewa maamuzi mwezi Januari, 2017.

Alisema mfumo huo mpya utapitisha timu 16 moja kwa moja kushiriki mashindano na zingine 32 zitacheza zenyewe kwa zenyewe na baada ya hapo timu 16 zitaungana na nyingine 16 ambazo zimeshafuzu na ndipo zitaingia katika hatua ya makundi.

“Wazo langu ni timu 16 zitafuzu hatua ya makundi na 32 zitashindana kutafuta timu zingine za kufuzu, watacheza katika nch ambayo Kombe la Dunia litakuwa linachezwa, watacheza kutafuta nafasi 16 zilizosalia,

“Ina maana tutaendelea na mfumo wa kawaida wa timu 32 kushiriki Kombe la Dunia, lakini timu 48 zitahusika na mashindano,” alisema Rais wa FIFA, Infantino.

Aidha mtandao wa Reuters umeripoti kuwa, pendekezo ambalo amelitoa Infantino linakubalika na Baraza la FIFA na kinachosubiriwa ni muda ufike ili maamuzi yatangazwe.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment